Ngonjera: Kubali Tu
KUBAKI TU Inawezekana ni mwenye usiri juu ya mabaya anayokufanyia mwenza wako. Lakini, bado ndugu, jamaa, marafiki wakawa wanajuwa kila kitu kuhusu yeye na, si ajabu wasikusaidie kwakuwa hawapendi uwe ni mwenye furaha kama wao au hata kuwazidi. zaidi wanapenda huzuni na majonzi yatawale moyoni mwako fikiria, ikiwa rafiki yako ndiye msaliti utafanyaje? Ikiwa ndugu yako au boss wako ndiye chanzo cha maumivu hayo utafanyaje? Usishangae wewe kuachwa au kuacha bali jiulize ni wapi unateleza hadi hayo yote yakukute , mhhhhhh… hata hivyo hakuna upendo unaodumu kwa kipimo kilekile cha awali. Kubali tu….. , Kubali tu kuwa huyo so wako tena Kubali tu kuwa huyo so yule wa kipindi kile , Kipindi kile cha ua changa , ua ambalo likifurahia kuchomoza kwa jua basi lilifurahia pia kuzama kwake Mmmmhhhhh ….. aaaaaaa haaaaa haaaaaaa. Labda pengine unajiuliza je, utawezaje kuishi bila yeye…. Maana kila ukitafakari unakosa majibu….. Huenda mtu huyo ni baba wa...