Ngonjera: Kubali Tu


KUBAKI TU

Inawezekana ni mwenye usiri juu ya mabaya anayokufanyia mwenza wako.

 Lakini, bado ndugu, jamaa, marafiki wakawa wanajuwa kila kitu kuhusu yeye

na, si ajabu wasikusaidie kwakuwa hawapendi uwe ni mwenye furaha kama wao au hata kuwazidi. zaidi wanapenda huzuni na majonzi yatawale moyoni mwako

fikiria, ikiwa rafiki yako ndiye msaliti utafanyaje? Ikiwa ndugu yako au boss wako ndiye chanzo cha maumivu hayo utafanyaje?

Usishangae wewe kuachwa au kuacha bali jiulize ni wapi unateleza hadi hayo yote yakukute , mhhhhhh… hata hivyo hakuna upendo unaodumu kwa kipimo kilekile cha awali.

Kubali tu….. ,

Kubali tu kuwa huyo so wako tena

Kubali tu kuwa huyo so yule wa kipindi kile , Kipindi kile cha ua changa , ua ambalo likifurahia kuchomoza kwa jua basi  lilifurahia pia kuzama kwake

Mmmmhhhhh ….. aaaaaaa haaaaa haaaaaaa.

 

Labda pengine unajiuliza  je, utawezaje kuishi bila yeye….

Maana kila ukitafakari unakosa majibu…..

Huenda mtu huyo ni baba wa watoto wako

Huenda mtu huyo ni mama wa watoto wako

Au huenda mtu huyo ni chanzo cha mafanikio yako.

Sikia,  fumbua macho….

Amka….,

fikiria kwa kina,  ikiwa wewe umeweza kuwa na hofu dhidi ya wema wake au umuhimu wake kwako.  je yeye alishindwaje kuujuwa umuhimu wako …

alishindwaje kuijua thamani yakooooo…. (kwa ukali)

Eti…?  alishindwaje kuutunza uaminifu wenu na hata akadiliki kukufanyia machafu anayokufanyia.

Ni mara ngapi amekuwa akirudia makosa yale yale kila mara ulipo msamehe.

Kwanini usimsahau.

Harafu….

Inashangaza sana, yaani kama unaweza kumsahau marehemu ilihali alikutoka ikiwa unamuhitaji, wakati anakuhitaji, ilihali wewe au yeye hakuna alojuwa ni nani atamtangulia mwenzie lakini bado uliweza kumsahau…..

Na je, vipi kuhusu huyo uliyemfumania mara kadhaa

Au Vipi huyo anayekuongopea kila siku…. au Mtu anayekupotezea muda wako , nguvu zako, mambo yako mengi yameharibika kisa yeye.

Unasindwaje kumsahau…

Mhh Mtu ambaye mmekutana tu ukubwani.

 

Tatizo hapa so kupigania penzi au kumpigania mtu bali cha muhimu hapa ni kuipigania furaha yako.

Huwezi kuwa na furaha wakati huna amani.

Na hauwezi kuwa na amani wakati uliyenaye si mwaminifu.

Na wala usije kujiaminisha kuwa raha za kimwili ni bora zaidi kuliko amani ya moyo .

Amka toka usingizini

Kubali kuwa huyo so type yako  tena

 

Afu kwa kifupi hakuna kitu kisichopokea mabadiliko kamwe….

Kila kitu huanza na huisha pia.

Amini tu kuwa upendo wenu umefika mwisho kabla ya kifo kuwatenganisha.

Nikukumbushe tu kuwa  hiyo ndoa yenu au uchumba wenu wa muda, isiwe sababu kwenu kushikilia yalopita, eti yanakufurahisha kila uyakumbukapo. Hapana…  huo ni ujinga.

Kumbuka,  ndoa ni sheria tu iliyowekwa kulinda mahusiano ya watu wanaopendana au mtu aliyependa hata kama yeye hajapendwa. Harafu…. Ndoa si ishara tosha ya upendo ama kujuwa kuwa watu fulani wanapendana…. Bali,  ni kifungo tu kama vifungo vingine. Vifungo ambavyo hata wasio na hatia hujikuta wakifungwa…

Wala Ndoa haiwezi kukupa uhuru wala nafasi ya kufanya marekebisho  juu ya usahihi wa chaguo lako

 Huwenda uliyenaye si chaguo sahihi kwako….

Je, Utafanya nini ikiwa uliye naye sasa si mwaminifu….

Etiii…. sema….

Utafanya nini…

Basi labda nikusaidie kujibu…

Muache……

Tena asirudi  kwenye maisha yako kamwe…..

Ikiwa unaweza kuishi bila wale ulowapenda kabla na hata ukayatoa maisha yako kwaajili yao kabla ya wao kufariki.  Je, unashindwaje kuishi bila huyo msaliti, tapeli, jambazi , tena mnafiki , mtu asiyeitambua thamani yako

Achana naye…

Narudia kusema   ….

Achana naye…

”Hakufai hata chembe mtu huyo”…

Naomba nimalize kwa kusema haya….

Siku zote upendo hutengenezwa

Kwa maana hiyo Upendo huzaliwa, hukuwa huishi  na hata kufa.

    ‘TUJIFUNZE KUSAHAU’’ ILI MAISHA MAPYA  YAENDELEE

 







   

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira