Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2024

Ngonjera: Hakuna Anayejali

Kalamu Ya Urithi Hakuna anayejali Siku yetu ni moja, jua letu ni moja na hata ardhi ni moja….. Wote tunazaliwa na tunakufa pia….. Lakini jiulize je, ni kwanini tutofautiane katika kuyaishi maisha….. Kwanini wengine waishi maisha ya ndoto zao   na wengine wasiyaishi… Wapo waliobahatika kuwa na furaha…… Wao huishi vile wanataka Kuanzia kula… kuvaaa.. kulala. .na hata kunywa… Furaha na   raha ni sehemu ya maisha yao.   Nani wakujali maisha anayoishi mtu huyu… mtu ambaye anasifa za kufika mahali fulani lakini hana refa wala sapport ya kumfanya afikie ndoto zake… Umasikini umeleta matabaka kiasi kwamba hata wanaouishi hawapendani… hawana umoja……. Wanaolewa hovyo…. Ni masikini… Wanaologana … ni masikini…. Wanaosengenyanya ni masikina Wanaofanyiana hila na choyo ni masikini Hivi kwa nini?

Ushairi: Kwaheri Mama

Kalamu Ya Urithi Kwakheri mama Ulipambana hukupenda kuniona Eti raha sina au nimenuna Dear mama… Leo Haupo nami tena Kweli Siwezi kukuona   Eeee maulana   Ni wewe mama uliyeshinda njaa Ili mwanao nipate kula Ni wewe mama uliyejinyima kuvaa Ili mwanao nipate pakulala   mama wewe ni shujaa     uliyekubali hasara uliyekaa jela mateso ya mitaala lakini hukuchoka na wala hukuwahi kuwa na hasira.   leo ardhi imekuita umeitika leo mwanao machoni umenitoka hivi ni nani tena shavuni atanishika nani huyo atakayekubali kuteseka asije sema amenichoka mama…   hivi kweli ndo umeondoka.     ulikunja hata ngumi Eti kisa mimi… Mama ujue siamini Nilikupenda sana lakini   kumbe yupo alokupenda zaidi yangu mimi.   Ungekuwepo mama ungenipenda zaidi yao Ungekuwepo mama ungejitoa kuliko wao Ungekuwepo mama usingekubali nichekwe nao.   Nakumbuka mama Hata nilipo umwa ...

Shairi: Nakumbuka

Kalamu Ya Urithi Nakumbuka Kila Nikikumbuka yale matendo Ukweli na wako upendo Mapigo ya moyo yanaongeza mwendo Nakumbuka zile skendo Nilipokupiga kwa nyundo Kisha nikakusukuma kando. Lakini bado haukunichoka…   Nakumbuka… Hata kipindi nilipokuforce kuachika Bado hukuwa tayari kuondoka   Nilipo   kuacha zaidi ya mwaka bado nyumbani hukutoka nakumbuka nilipo rudi nilikukuta tena umejipata ukawa unanibembeleza ukinituliza huku ukiniliwaza. Ukiamini nimebadilika   Nakumbuka Hata mwili wangu haukuwahi kuushika Hata uliponitaka Nilidai nimechoka Usiku ulipofika Nilitoroka Ila bado hukunichoka..   Nakumbuka Ulilia kwa huruma Huku Ukionesha moyo unavyouma Maneno ya huzuni ukiyasema Moyo mkuki nauchoma.   Nakumbuka Kwa sauti ya kukwama Pumzi nzito ukihema… Ukidai nikuonee huruma   Daah Sikukwelewa… Maana tayari nilikuwa nimelewa Nakumbuka Bila huruma makofi na mateke ni...

Shairi: Moyo Wa Subira

Kalamu Ya Urithi Moyo wa subira   Subira hurejesha furaha iliyopotea Moyo wenye subira daima hauwezi teketea. Daima ni wenye kukuwa na kuendelea  Moyo dhaifu hauachi kupendelea   Moyo ulopenda ni kawaida kuumia Ndiyo maana hauchoki kuvumilia   Upendo haujaribiwi kamwe Wala Penzi so shamba eti mwaka huu lisilimwe Mapenzi ni bustani  ili itembelewe ipendwe Ni lazima isafishwe na itunzwe   Halafu .. Kwenye haya maisha wewe ni nani hadi usisemwe Kwenye mapenzi haya wewe ni nani hadi usiumizwe Wewe ni nani eti muda wote upendwe… Usinyimwe…. Usiachwe…. usifiwe… Kumbuka So kila kitu kipo kwa ajili yako wewe. Vingine vina wenyewe   Wapo lakini so kila mtu ataguswa nawe Bali upendo wa kweli huanza ndano yako mwenyewe   Na Kwenye maisha yako usitegemee kupendwa na asokujuwa Hivyo wape nafasi wengine kukuelewa Kwa maana upendo wa kweli hutoka kwa wanaokutambuwa wakakuelewa.   Uaminifu ni akiba ...

Shairi: Unakumbuka ?

Kalamu Ya Urithi  Unakumbuka?   Unakumbuka eee….. Kipindi kile unadate nae….. Unakumbuka eee… Kipindi kile umeziteka hisia zake… Ukamfanya apoteze hamu ya kula kisa wewe… Usingizi asiupate kisa wewe…. Unakumbuka lakini….. Kipindi kile mwenzio alipoyatoa maisha yake kwa ajili yako…. yeye alipojinyima ili wewe upate… Unakumbuka….. Lakini leo hauko naye tena…..   Nikukumbushe kitu…. Unakumbuka kipindi kile mlipokuwa mkitoka out Mkienda garden Mara ufukweni…. Mkiwa barabarani..   mlifurahi na kucheka sana….   Mlifikia hatua mkawa kama machizi vile machoni mwa watu. Ila mlipendeza sana. Unazikumbuka kweli hizo moment….. Masikini….   leo hauko naye tena. Mhhh aaaaaaa…….   Hivi unakumbuka kipindi kile mnachati usiku kucha …. eeee ….. eti mnaongea na simu masaa 10 mhhh…. Mara utasikia kata weweeee bhanaaa Mhh mhhm takiii kata wewe…. Ka watoto vile Ha ha ha ha ha ha ha Aiseee… Vp unakumbuka kwe...

Ngonjera: Ya Duniani

Kalamu Ya Urithi Ya duniani   Huwenda hukuwa na utambuzi mzuri juu ya ile kauli isemayo kuwa uyaone. Huenda ni utoto tu na ujinga wa kipindi kile   ukiwa mdogo na ndiyo maana uliamini kuwa siku ukiwa mkubwa utakuwa na maisha mazuri. utakuwa ni mtu maarufu sana, na utapendwa karibu na kila mtu, utasaidia kila mwenye uhitaji. Na kubwa kuliko utakuwa na mpenzi mzuri mwenye kumjali na hata mkawa ni watu wenye kupendana sana. Lakini kumbe haiko hivyo…. Mambo hubadilika siku hadi siku. Na hata hivyo haikuwa rahisi kwa wewe kuamua ni aina gani ya maisha uyaishi ili hali wakati huo ulikuwa nimdogo sana na kwa bahati mbaya haukuwa na nafasi ya kufanya maamuzi kwa wakati huo. Zaidi ulikuwa ni tegemezi kwa kila kitu kipindi chote cha makuzi yako hadi kufikia sasa. Na sasa ni ni mtu mzima…. Unajuwa baya ni lipi na lipi ni zuri…. Kwa sababu hiyo, hatima ya maisha yako ya baadae huwa yapo mikononi mwa walezi wako. Hata maisha unayoishi leo ni juhudi za walezi wak...

Ngonjera: Kubali Tu

KUBAKI TU Inawezekana ni mwenye usiri juu ya mabaya anayokufanyia mwenza wako.  Lakini, bado ndugu, jamaa, marafiki wakawa wanajuwa kila kitu kuhusu yeye na, si ajabu wasikusaidie kwakuwa hawapendi uwe ni mwenye furaha kama wao au hata kuwazidi. zaidi wanapenda huzuni na majonzi yatawale moyoni mwako fikiria, ikiwa rafiki yako ndiye msaliti utafanyaje? Ikiwa ndugu yako au boss wako ndiye chanzo cha maumivu hayo utafanyaje? Usishangae wewe kuachwa au kuacha bali jiulize ni wapi unateleza hadi hayo yote yakukute , mhhhhhh… hata hivyo hakuna upendo unaodumu kwa kipimo kilekile cha awali. Kubali tu….. , Kubali tu kuwa huyo so wako tena Kubali tu kuwa huyo so yule wa kipindi kile , Kipindi kile cha ua changa , ua ambalo likifurahia kuchomoza kwa jua basi  lilifurahia pia kuzama kwake Mmmmhhhhh ….. aaaaaaa haaaaa haaaaaaa.   Labda pengine unajiuliza  je, utawezaje kuishi bila yeye…. Maana kila ukitafakari unakosa majibu….. Huenda mtu huyo ni baba wa...