Ngonjera: Ya Duniani

Kalamu Ya Urithi




Ya duniani 

Huwenda hukuwa na utambuzi mzuri juu ya ile kauli isemayo kuwa uyaone.

Huenda ni utoto tu na ujinga wa kipindi kile  ukiwa mdogo na ndiyo maana uliamini kuwa siku ukiwa mkubwa utakuwa na maisha mazuri.

utakuwa ni mtu maarufu sana, na utapendwa karibu na kila mtu,

utasaidia kila mwenye uhitaji.

Na kubwa kuliko utakuwa na mpenzi mzuri mwenye kumjali na hata mkawa ni watu wenye kupendana sana.

Lakini kumbe haiko hivyo….

Mambo hubadilika siku hadi siku.

Na hata hivyo haikuwa rahisi kwa wewe kuamua ni aina gani ya maisha uyaishi ili hali wakati huo ulikuwa nimdogo sana na kwa bahati mbaya haukuwa na nafasi ya kufanya maamuzi kwa wakati huo.

Zaidi ulikuwa ni tegemezi kwa kila kitu kipindi chote cha makuzi yako hadi kufikia sasa.

Na sasa ni ni mtu mzima….

Unajuwa baya ni lipi na lipi ni zuri….

Kwa sababu hiyo, hatima ya maisha yako ya baadae huwa yapo mikononi mwa walezi wako.

Hata maisha unayoishi leo ni juhudi za walezi wako.

Iwe ni kwenye mahusiano au hata katika shughuli za utafutaji bado walezi wako ndiyo wenye kuashiria hatima ya maisha yako.

Maana wao ndiyo wenye kukuandalia msingi wako wa maisha…

Hapa niwape pole wale mlio na walezi ama wazazi wasiojitambua yaani vilaza…

Maana mzazi mwenye kujielewa hawezi kushinda baa au kutwa akibadili wachumba, au mama kutwa kubadili mitindo ya nywele na manukato ya bei ghali

ili hali kizazi chake kinahangaika’’’

kinataabika…

mzazi unashindania fashion za nguo, pikipiki,magari, namatoleo ya simu.

Na wakati huo  damu yake, mtoto wake, kijana wake  hana kazi hana mtaji wala hajui afanye nini.

Kuna wazazi,  ni bora aweke bando la bukumbili au tatu ili akeshe mtandaoni akichat lakini wakati huo mtoto wake hana vifaa vya shule.

Huenda wewe hapo unapitia magumu hayo  kwa sababu tu  jana yako haikuwa nzuri…

Ndiyo…

 jana yako haikuandaliwa vizuri  na watangulizi wako.

Tazama…. leo hii mahusiano yako yanashida kwa sababu huwenda umekulia katika malezi ya aina hiyo….

Baba mama hugombana hadharani….

Ukiwa mtoto huenda ulikuwa huku ukijuwa machafu ya tabia za wazazi wako.

Mtoto mdogo kushirikishwa katika matukio kama usaliti, wizi, umbea , na hata uongo .

Lakini haujachelewa….

Matendo na tabia chafu zitaathiri maisha yako kwasababu ya uamuzi wako.

Uamuzi utakaouchukuwa leo ili kuisahihisha kesho yako kutokana na makosa uliyokwisha kufanyIka jana.

 

Chini ya jua

 akitakacho mwelevu kiwe, basi kinawezekana kuwa

 

Hatufanikiwi kwasababu tunawekeza katika kushindwa

wamefanikiwa kwa sababu hapo kabla walianguka mara kadhaa… na waliwekeza katika kufanikiwa.

hivyo mimi nawewe tunapaswa kupitia mchakato huo.

Mchakato ambao huenda ukaghalimu hata uhai wako…

 

Kuna kipindi utagombana na kila mtu…

Kipindi hicho utapoteza kila ulichokipenda…

Kila kitu kwako kitabaki kuwa historia…

Na hapo ndipo utaanza kuingia katika majaribu ya hapa duniani.

Kama ni chungu ya maisha basi hapa ndipo utaijuwa….

Na hata ile kauli ya dunia duara basi hapa ndipo mahala pake…

Aisee tujifunze kuyaheshimu na kuyazingatia maneno ya watangulizi wetu yaani wahenga.

Ama kwa hakika wakati huo hutakaa ukausahau kamwe

Wakati ambao utabaki kama msindikizaji tu wa mafanikio ya wenzako….

Utakuwa na wakati mgumu kiasi cha kujichukia…

Wakati ambao utapaswa kukubaliana na kila hali

Wakati ambao utapitia kila aina ya shida…

Tabu

Maumivu

Dharau,

Lakini huwezi amini hicho ndo kipindi cha mimi na wewe kuweza kusimama tena

Hicho ndo kipindi cha wewe na mimi kurekebisha tulipokosea..

Kipindi ambacho kila kitu kitapaswa kuanza upya.

Uzima ni zawadi  ama ahadi isiyo na matumaini ndani yake

Kwani unaweza usiipate zawadi hiyo.

Na kama ahadi hiyo itatimia basi kuna kila sababu ya kuwa watumiaji wazuri wa ahadi hiyo.

Hivi unatambua ya kuwa maisha haya bila wewe hayawezi kunoga…

Tena kama ni chakula basi hakitakuwa na radha hata kidogo.

Raha ya maisha uishi sambamba na wengine… uishi ukiona wengine wanaishi…. Wakuone ukifurahia… uwaone wakifurahia pia.

Ukitembea kama wao… ukilala kama wao… ukiamka kama wao… ukipumua kama wao…. Yaani wakuone uwaone.

Na ikitokea wewe uko na fura wao hawana hapo raha haitakuwepo…

Maana furaha ya moyo hutegemea sana amani ya watu wakuzungukao.

Kwa maana hiyo kasoro moja katika yote yaletayo uzima basi matokeo yake ni huzuni na hapo maisha yako yatakuwa yameingiwa na dosari.


Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira