Shairi: Kipenzi changu

 



Kipenzi changu

Halooo…

Halooo…

Chozi hili lanibugujika,

Ni kwasababu nimekukumbuka,

Sakura aaaa….. mamaa  afriaka,

Si kwa ukimya  huo,

unanifanya niumie mwenzio,

Sakuraa wewe ndo langu kimbilio,

Kwa mwingine sioni singizio.

 

Nimeyafunga yangu macho,

Ili tu nisitamani vipitacho,

Hakuna kinitesacho,

 zaidi ya penzi lako,

Hakika ndani ya huu moyo,

uko peke yako.

 

Sakura kipenzi…

Naomba nivumilie kwa kipindi hiki,

Nyakati iliyojaa shida na dhiki,

ukidhani siwakumbuki,

Au pengine nadhihaki

Mama afriki.

 

Kila siku napiga goti chini,

nikinyoosha mikono yangu juu,

nikikuombea furaha na amani,

nikiomba mungu aulinde upendo huu.

 

Najuwa pesa ndo kimbilio la kila mtu,

Ila tafadhari usije niacha peke yangu,

Ukawafuata wenye vitu,

Ukaniacha mimi kapuku nikilia kwa machungu.

 

Najuwa mbali nipo,

Hasa na upeo wa mboni za yako macho,

Ila tambua,

Popote ulipo nami nipo,

Mfano wa giza na popo.

 

Kuna wakati namiss uwepo wako,

Kuna wakati namiss penzi lako..

Ile michezo yako…

Mideko na yale malingo,

Tukiimba na kurushiana mito,

Yaani kama watoto.

 

Haikuwa tomato,

Haikuwa avocado,

Bali ni upendo,

Ndiyo unipao haya mawazo.

 

Ikiwa umbali ni sumu ya penzi,

Basi kuonana ndo tiba pekee,

Ikiwa bila wewe kuishi siwezi,

Basi penzi langu niwekee.

 

Na kama kupenda ni uchizi,

Basi acheni nipotee,

Lakini kukuacha siwezi,

Amini wewe ndo wangu wa pekee.

 

Najuwa utakuwa na hasira,

Najuwa unahitaji hela,

Naelewa huwezi lala bila kula,

Najuwa umechoshwa na huu ufukara.

 

Naelewa kuna time unajiona fara,

Na vile sina ajira,

Unahisi umepata hasara,

Unahisi umepoteza dira.

 

Naomba mpenzi tafadhari,

Penzi letu usije liweka kando,

Naomba kwa hili jihadhari,

Afriq wangu mfunze upendo.

 

Kamwe usiwe mbali,

Mfunze kuhusu uzalendo,

Sitopenda awe na kiburi,

Naomba ichunge mienendo.

 

Tena lisimamie hili,

Asifiwe kwa uzuri wa matendo,

Muandae kuwa na akili,

Hakikisha anacheza nawe kando,

Muweke mbali na michezo ya magendo.


na Kilimboka

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Moyo Wa Subira