Shairi : Chini Ya Jua

Kalamu Ya Urithi



Chini ya Jua

Chini ya jua

Kunawatu wanaishi kwa kutegemea dhiki za watu…

Kwao utu si kitu

Kwao pesa ndo kila kitu.

 

Ni chini ya jua….

Mengi utayatambua

Huko hakuna siri kila kitu ni dhahili..


Chini ya jua….

Huku ukitaka kumjua asiyekupenda

Basi patwa na shida…

 

Chini ya jua

Kuna viumbe hupenda kuishi kuliko kufa

Uzushi kuliko taarifa

Raha kuliko tabu….

Chungu kuliko tamu


Huko chini ya jua

Vya haramu ndivyo vinaumuhimu….


Chini ya jua

Watu wanapenda uzinzi kuliko kazi…

Watoto wa nje ni wengi kuliko wa ndani.

Akiba ni ndogo kuliko madeni.

 

Chini ya jua

rushwa ni bora kuliko kula

Huku wengi huamini sana kulogwa kuliko kugongewa

Wengi wao ni wazawa waliojiweka utawa

Huona raha wakisifiwa

Hawaoni ajabu wakidaiwa.

 

Chini ya jua…

Kuna viumbe wa ajabu sana

Hawa aibu hawana..

Wao kwa wao huchapana

Mikia kulishana

Nyonga kushikana

Hawachelewi mapajani kuwekana.


Chini ya jua.

Litokealo lea afadhari ya jana.

 

Chini ya jua

Huko bhana ndoa so kikwazo

Eti utaondosha mawazo

Huko ndoa ni likizo

Tena pango la kuficha uozo

Kimbilio pekee la watu waroho na waongo.

 

Chini ya jua

Kuna viumbe wanaimani kuliko hata wanaye muamini….

Huku kuna viumbe wanaogopwa kuzidi hata maanani.


Chini ya jua

Kuna people Hawana kazi lakini wanalipwa..

Hawana hadhi lakini wanalindwa

Hawana mioyo lakini bado wanapendwa

Daaaaaa…

Wao kucheka  hadi wakuone ukilia

Wao kununa hadi wakuone ukiendelea.

 

Huko chini ya jua…

Kuacha kuachwa ni jambo la kawaida…

Wanaamini hakuna danga lisilo na faida

Wala buzi lisilochunika….

Huko ukila nawe juwa umelika

Ukilia usitarajie kucheka

Ukipenda jiandae kuachika

Na kama ukipendwa basi jiandae kutajirika.

 

Huko chini ya jua

Kuna nishati lakini hawana mwanga….

Asubuhi jua  mchana majanga

Mchana dua jioni kipenga.

 

Huko chini ya jua

Kuna visoke wabeba unga

Kuna makundi ya wanga kuliko waganga

Mabibi washika nyanga, mafundi  wa kuchezea anga.

 

Chini ya jua

Huko walinzi hawajui kupiga kipenga

Zaidi wa migambo kushika mapanga

Kusumbua wanaopanga.

Wenye nyumba walojenga.

 

Huko chini ya jua

Wanamaisha ya ajabu sana

Yaani wana vyanzo vya maji

Lakini nguvu ya kuoga hawana

Wanamifereji lakini ndoo hawakingi

Wanachemchem lakini misingi hawajengi

Hawana kiu  wanaokufa ni wengi.

 

Huko chini ya jua.

Kuna wasomi wengi kupindukia

Wasio na haki wasio na hatia

tena ni wachache walio na njia

Wengi wao hawajui wapi pakuanzia.

 

Chini ya jua

Huko hakuna kigeni

Wala habari ya amani

Huko mauaji ni hadharani

Si ya dereva wala hayawani

Milipuko ya vimondo na volkani.

 

Huko chini ya jua

Kila mtu anataka usikani

Nae aingie barabarabarani

Huko chini ya jua

Eti ukijifanya unajua

So ajabu wakakwanua

’CHINI YA JUA’’


na Kilimboka

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira