Kubali tu kuwa huyo siyo wako tena
KUBALI TU
Inawezekana
ni mwenye usiri juu ya mabaya anayokufanyia mwenza wako.
Lakini, bado ndugu, jamaa, marafiki wakawa
wanajuwa kila kitu kuhusu yeye
na, si ajabu
wasikusaidie kwakuwa hawapendi uwe ni mwenye furaha kama wao au hata kuwazidi.
zaidi wanapenda huzuni na majonzi yatawale moyoni mwako
fikiria,
ikiwa rafiki yako ndiye msaliti utafanyaje? Ikiwa ndugu yako au boss wako ndiye
chanzo cha maumivu hayo utafanyaje?
Usishangae
wewe kuachwa au kuacha bali jiulize ni wapi unateleza hadi hayo yote yakukute ,
mhhhhhh… hata hivyo hakuna upendo unaodumu kwa kipimo kilekile cha awali.
Kubali tu…..
,
Kubali tu
kuwa huyo so wako tena
Kubali tu
kuwa huyo so yule wa kipindi kile , Kipindi kile cha ua changa , ua ambalo
likifurahia kuchomoza kwa jua basi
lilifurahia pia kuzama kwake
Mmmmhhhhh
….. aaaaaaa haaaaa haaaaaaa.
Labda
pengine unajiuliza je, utawezaje kuishi
bila yeye….
Maana kila
ukitafakari unakosa majibu…..
Huenda mtu
huyo ni baba wa watoto wako
Huenda mtu
huyo ni mama wa watoto wako
Au huenda
mtu huyo ni chanzo cha mafanikio yako.
Sikia, fumbua macho….
Amka….,
fikiria kwa
kina, ikiwa wewe umeweza kuwa na hofu
dhidi ya wema wake au umuhimu wake kwako.
je yeye alishindwaje kuujuwa umuhimu wako …
alishindwaje
kuijua thamani yakooooo…. (kwa ukali)
Eti…? alishindwaje kuutunza uaminifu wenu na hata
akadiliki kukufanyia machafu anayokufanyia.
Ni mara
ngapi amekuwa akirudia makosa yale yale kila mara ulipo msamehe.
Kwanini
usimsahau.
Harafu….
Inashangaza
sana, yaani kama unaweza kumsahau marehemu ilihali alikutoka ikiwa unamuhitaji,
wakati anakuhitaji, ilihali wewe au yeye hakuna alojuwa ni nani atamtangulia
mwenzie lakini bado uliweza kumsahau…..
Na je, vipi
kuhusu huyo uliyemfumania mara kadhaa
Au Vipi huyo
anayekuongopea kila siku…. au Mtu anayekupotezea muda wako , nguvu zako, mambo
yako mengi yameharibika kisa yeye.
Unasindwaje
kumsahau…
Mhh Mtu
ambaye mmekutana tu ukubwani.
Tatizo hapa
so kupigania penzi au kumpigania mtu bali cha muhimu hapa ni kuipigania furaha
yako.
Huwezi kuwa
na furaha wakati huna amani.
Na hauwezi
kuwa na amani wakati uliyenaye si mwaminifu.
Na wala
usije kujiaminisha kuwa raha za kimwili ni bora zaidi kuliko amani ya moyo .
Amka toka
usingizini
Kubali kuwa
huyo so type yako tena
Afu kwa
kifupi hakuna kitu kisichopokea mabadiliko kamwe….
Kila kitu
huanza na huisha pia.
Amini tu
kuwa upendo wenu umefika mwisho kabla ya kifo kuwatenganisha.
Nikukumbushe
tu kuwa hiyo ndoa yenu au uchumba wenu
wa muda, isiwe sababu kwenu kushikilia yalopita, eti yanakufurahisha kila
uyakumbukapo. Hapana… huo ni ujinga.
Kumbuka, ndoa ni sheria tu iliyowekwa kulinda
mahusiano ya watu wanaopendana au mtu aliyependa hata kama yeye hajapendwa.
Harafu…. Ndoa si ishara tosha ya upendo ama kujuwa kuwa watu fulani
wanapendana…. Bali, ni kifungo tu kama
vifungo vingine. Vifungo ambavyo hata wasio na hatia hujikuta wakifungwa…
Wala Ndoa
haiwezi kukupa uhuru wala nafasi ya kufanya marekebisho juu ya usahihi wa chaguo lako
Huwenda uliyenaye si chaguo sahihi kwako….
Je, Utafanya
nini ikiwa uliye naye sasa si mwaminifu….
Etiii….
sema….
Utafanya
nini…
Basi labda
nikusaidie kujibu…
Muache……
Tena
asirudi kwenye maisha yako kamwe…..
Ikiwa
unaweza kuishi bila wale ulowapenda kabla na hata ukayatoa maisha yako kwaajili
yao kabla ya wao kufariki. Je,
unashindwaje kuishi bila huyo msaliti, tapeli, jambazi , tena mnafiki , mtu
asiyeitambua thamani yako
Achana naye…
Narudia
kusema ….
Achana naye…
”Hakufai
hata chembe mtu huyo”…
Naomba
nimalize kwa kusema haya….
Siku zote
upendo hutengenezwa
Kwa maana
hiyo Upendo huzaliwa, hukuwa huishi na
hata kufa.
‘’TUJIFUNZE KUSAHAU’’ ILI MAISHA MAPYA YAENDELEE.
Maoni