Ngonjera: Hakuna Anayejali
Kalamu Ya Urithi Hakuna anayejali Siku yetu ni moja, jua letu ni moja na hata ardhi ni moja….. Wote tunazaliwa na tunakufa pia….. Lakini jiulize je, ni kwanini tutofautiane katika kuyaishi maisha….. Kwanini wengine waishi maisha ya ndoto zao na wengine wasiyaishi… Wapo waliobahatika kuwa na furaha…… Wao huishi vile wanataka Kuanzia kula… kuvaaa.. kulala. .na hata kunywa… Furaha na raha ni sehemu ya maisha yao. Nani wakujali maisha anayoishi mtu huyu… mtu ambaye anasifa za kufika mahali fulani lakini hana refa wala sapport ya kumfanya afikie ndoto zake… Umasikini umeleta matabaka kiasi kwamba hata wanaouishi hawapendani… hawana umoja……. Wanaolewa hovyo…. Ni masikini… Wanaologana … ni masikini…. Wanaosengenyanya ni masikina Wanaofanyiana hila na choyo ni masikini Hivi kwa nini?