Ushairi: Kwaheri Mama

Kalamu Ya Urithi



Kwakheri mama


Ulipambana

hukupenda kuniona

Eti raha sina au nimenuna

Dear mama…

Leo Haupo nami tena

Kweli Siwezi kukuona

 

Eeee maulana

 

Ni wewe mama uliyeshinda njaa

Ili mwanao nipate kula

Ni wewe mama uliyejinyima kuvaa

Ili mwanao nipate pakulala

 mama wewe ni shujaa

 

 

uliyekubali hasara

uliyekaa jela

mateso ya mitaala

lakini hukuchoka na wala

hukuwahi kuwa na hasira.

 

leo ardhi imekuita umeitika

leo mwanao machoni umenitoka

hivi ni nani tena shavuni atanishika

nani huyo atakayekubali kuteseka

asije sema amenichoka

mama…

 hivi kweli ndo umeondoka.

 

 ulikunja hata ngumi

Eti kisa mimi…

Mama ujue siamini

Nilikupenda sana lakini

 kumbe yupo alokupenda zaidi yangu mimi.

 

Ungekuwepo mama ungenipenda zaidi yao

Ungekuwepo mama ungejitoa kuliko wao

Ungekuwepo mama usingekubali nichekwe nao.

 

Nakumbuka mama

Hata nilipo umwa

Ulilia sana

Kifua kilikujaa

Kando yangu ulikaa

Hata ukashinda njaa

Masaa hadi masaa

 

Dear mama

Hivi kweli tutakutana

Au ndo tutapishana

Hatutaonana

 

 ilikuwa jana

mbona ghafla sana

mara ya mwisho kuwa_siliana

yaani kama nakuona…

 

nilipokosea ulinikemea

nilipoonewa ulinitetea

niliporejea ulinipokea

 

mama leo upweke umeniachia….

vipi moyo utatulia

Mwili nguvu imeniishia

Ooo huzuni imeniingia

 

Ujuwe mama….

Sikuwahi fikiria

Kuwa siku  itafikia

Safari njiani utaishia

leo mpweke nimebakia

 

Dear mama

Nitawezaje kuzoea

ili hali uko mbali

nashindwa kuelezea

ulivyo mwema na mkweli

 

hukuwahi kuniongopea

ulonitendea ni mazuri

mahala pema nakuombea

malaika wa pepo akukubali

aweze kukupokea

pasina dosari.

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira