Shairi: Moyo Wa Subira

Kalamu Ya Urithi




Moyo wa subira

 

Subira hurejesha furaha iliyopotea

Moyo wenye subira daima hauwezi teketea.

Daima ni wenye kukuwa na kuendelea

 Moyo dhaifu hauachi kupendelea

 

Moyo ulopenda ni kawaida kuumia

Ndiyo maana hauchoki kuvumilia

 

Upendo haujaribiwi kamwe

Wala Penzi so shamba eti mwaka huu lisilimwe

Mapenzi ni bustani  ili itembelewe ipendwe

Ni lazima isafishwe na itunzwe

 

Halafu ..

Kwenye haya maisha wewe ni nani hadi usisemwe

Kwenye mapenzi haya wewe ni nani hadi usiumizwe

Wewe ni nani eti muda wote upendwe…

Usinyimwe…. Usiachwe…. usifiwe…

Kumbuka So kila kitu kipo kwa ajili yako wewe.

Vingine vina wenyewe

 

Wapo lakini so kila mtu ataguswa nawe

Bali upendo wa kweli huanza ndano yako mwenyewe

 

Na Kwenye maisha yako usitegemee kupendwa na asokujuwa

Hivyo wape nafasi wengine kukuelewa

Kwa maana upendo wa kweli hutoka kwa wanaokutambuwa wakakuelewa.

 

Uaminifu ni akiba yenye kuhitaji matunzo

Japo upendo wa kweli huonekana mwanzo

Hata hivyo

Penzi  so pishi utake kionzo

Kwa maana utamu wa chakula haushibishi tumbo

Chunga sana usije kuwa chambo

Usije sakamia mapenzi kwa kufuata mkumbo.

 

Moyo ulokufa daima hausikii dawa

Na siku zote ukikataliwa

Basi tambuwa umechelewa

Na kama siyo basi huenda mtu huyo hajakuelewa

 

Kwa maana kupendwa nikubalikiwa

Kupendwa ni kupendelewa

Kupendwa ni kuaminiwa

Kupendwa ni kukubaliwa

 

 

Hakuna haja ya wewe kunung’unika

Eti mtu furani amebadilika

Eti mtu furani amekuchoka

Kwa maana akupendaye hakika

Daima atakushika

Huyo ni wa kufa na kuzika

 

Unachokipenda kamwe hakilingani na unachokitaka.

Kwa maana upendo haupimwi kwa kushika

upendo ni rangi isiyobadilika

Upendo ni kumbukumbu isiyoweza kufutika

Hivyo chunga usije ichoka

Kwa maana upendo huja na kuondoka.

Upendo ni amali inayohitajika kutunzika

Upendo ni sawa na vita ipigwanayo bila kuchoka

 

Mapenzi bahari

Ikiwa safi ni mazuri

Ikiwa chafu ni hatari

 

Mapenzi ni  kama chai

Ikikos sukari haifai

Ikiwa nayo utafurahi

 

Mapenzi so kiu ya maji

Eti ukiyapata imetosha

Wala so bakuli la uji

Eti ukipoa umekomesha

Na mapenzi si vita ya miji

 eti uipigane ikaisha

wala  mapenzi so mtaji

eti ukiupata basi umewin maisha.

 

Unaweza kuipata ndoa na si furaha

Unaweza usiwe na doa lakni ukawa na jeraha

Unaweza kujikomboa lakini usiishi kwa raha

Unaweza kumtoboa  lakini  usimtoe usaha

Siku zote anaye kukomoa usimletee mzaha

Lengo langu so kubomoa ila kutoa nasaha.



Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu