Shairi: Nakumbuka

Kalamu Ya Urithi




Nakumbuka


Kila Nikikumbuka yale matendo

Ukweli na wako upendo

Mapigo ya moyo yanaongeza mwendo

Nakumbuka zile skendo

Nilipokupiga kwa nyundo

Kisha nikakusukuma kando.

Lakini bado haukunichoka…

 

Nakumbuka…

Hata kipindi nilipokuforce kuachika

Bado hukuwa tayari kuondoka

 

Nilipo  kuacha zaidi ya mwaka

bado nyumbani hukutoka

nakumbuka

nilipo rudi nilikukuta

tena umejipata

ukawa unanibembeleza

ukinituliza

huku ukiniliwaza.

Ukiamini nimebadilika

 

Nakumbuka

Hata mwili wangu haukuwahi kuushika

Hata uliponitaka

Nilidai nimechoka

Usiku ulipofika

Nilitoroka

Ila bado hukunichoka..

 

Nakumbuka

Ulilia kwa huruma

Huku Ukionesha moyo unavyouma

Maneno ya huzuni ukiyasema

Moyo mkuki nauchoma.

 

Nakumbuka

Kwa sauti ya kukwama

Pumzi nzito ukihema…

Ukidai nikuonee huruma

 

Daah

Sikukwelewa…

Maana tayari nilikuwa nimelewa

Nakumbuka

Bila huruma makofi na mateke nilikupiga

Huku nikitoa sauti kali yakukuswaga…

Usiku huo sikumbuki wapi ulilalaga

 

Nakumbuka

Unyama nilio kufanyia

ile siku ulipo nifumania

tena kwenye kitanda tunacho lalia..

nakumbuka sana uliumia

sana ulilia..

lakini bado hukuwahi kunichukia

 

 

nakumbuka

kosa nifanye mimi

ajabu msamaha uliomba wewe

furaha kwakwo ilikuwa simulizi na visawe

niliyekufanya mwewe mpigwa mawe

 

mwanamke mvumilivu

tena mkakamavu asiye na wivu

niliyekupaka majivu

na kukufunga nyavu…

 

nakumbuka

si kwa mateso niliyokupa

viboko nilivyokuchapa

nikakuita kahaba

eti mwizi wa kuiba

shingo nilikukaba

pua nikakuziba..

kiasi cha kuleta msiba.

 

daaah

lakini bado hukuchoka kunipenda…

 

tazama leo

sina maendeleo

sina tegemeo

sina upendeleo

wala sina mwelekeo

naishia kuulizwa yuko wapi mkeo

nakumbuka

 

ni kama nakuona vile ukiwa jikoni

na sahani mkononi

mwanamke mcheshi

 tena hodari wa mapishi

ulijua kupambana ili tuishi

hukuwa wa dharau wala kashikashi

 

 nakumbuka ule wema wako

japo

 kuwa sikuijuwa thamani yako

tazama leo nalipa chozi lako

na leo nashuhudia kifo chako

kwanini uliniruhusu niuumize nafsi yako

kwanini sikubakia upande wako

 

nakumbuka

ulinipenda sana….

Uliumia tulipogombana…

Ulifurahi tulipokumbatiana

Ulipenda kuona tukishirikiana.

 

Sasa kwanini hayo yote sikuyaona..

Leo peke yangu nang’ang’ana

Hakuna anayeniona

Hata majirani tumekosana

 

Sina tena wa kuniamini

Wala wa kunithamini

Kumbe sikupendwa walinitamani

Laiti ningelijuwa ya mbeleni

Nisingeruhusu haya yajitokeze abadani

Kwa maana yananinyima amani

Yananiumiza rohoni.

 

Ona sasa ndo hivyo unakwenda

Mwanamke pekee uliyenipenda

Uliyepigana kunilinda

Penzi kubaya lisije enda

Kumbe ubaya mwenyewe niliupanda

takukumbuka

 

Hivi ndo kweli unaundoka

Au naota….

Hivi kweli unanitoka

Inamaa tena sitakupata

Natamani niweze hata kukushika

Natamani tena uweze niita

Kwaheshima niweze kuitika….

 

sasa kwanini sikujuwa haya.

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira