Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 17, 2023

Ushairi : Unakumbuka ?

Kalamu Ya Urithi Unakumbuka? Unakumbuka eee….. Kipindi kile unadate nae….. Unakumbuka eee… Kipindi kile umeziteka hisia zake… Ukamfanya apoteze hamu ya kula kisa wewe… Usingizi asiupate kisa wewe…. Unakumbuka lakini... Kipindi kile mwenzio alipoyatoa maisha yake kwa ajili yako…. yeye alipojinyima ili wewe upate… Unakumbuka….. Lakini leo hauko naye tena…..   Nikukumbushe kitu…. Unakumbuka kipindi kile mlipokuwa mkitoka out Mkienda garden Mara ufukweni…. Mkiwa barabarani..  mlifurahi na kucheka sana….   Mlifikia hatua mkawa kama machizi vile machoni mwa watu. Ila mlipendeza sana. Unazikumbuka kweli hizo moment….. Masikini….  leo hauko naye tena. Mhhh aaaaaaa…….   Hivi unakumbuka kipindi kile mnachati usiku kucha …. eeee ….. eti mnaongea na simu masaa 10 mhhh…. Mara utasikia kata weweeee bhanaaa Mhh mhhm takiii kata wewe…. Ka watoto vile Ha ha ha ha ha ha ha Aiseee… Vp unakumbuka kweli hizo moment…...

Kubali tu kuwa huyo siyo wako tena

Kalamu Ya Urithi KUBALI TU Inawezekana ni mwenye usiri juu ya mabaya anayokufanyia mwenza wako.   Lakini, bado ndugu, jamaa, marafiki wakawa wanajuwa kila kitu kuhusu yeye na, si ajabu wasikusaidie kwakuwa hawapendi uwe ni mwenye furaha kama wao au hata kuwazidi. zaidi wanapenda huzuni na majonzi yatawale moyoni mwako fikiria, ikiwa rafiki yako ndiye msaliti utafanyaje? Ikiwa ndugu yako au boss wako ndiye chanzo cha maumivu hayo utafanyaje? Usishangae wewe kuachwa au kuacha bali jiulize ni wapi unateleza hadi hayo yote yakukute , mhhhhhh… hata hivyo hakuna upendo unaodumu kwa kipimo kilekile cha awali. Kubali tu….. , Kubali tu kuwa huyo so wako tena Kubali tu kuwa huyo so yule wa kipindi kile , Kipindi kile cha ua changa , ua ambalo likifurahia kuchomoza kwa jua basi   lilifurahia pia kuzama kwake Mmmmhhhhh ….. aaaaaaa haaaaa haaaaaaa.   Labda pengine unajiuliza   je, utawezaje kuishi bila yeye…. Maana kila ukitafakari unakosa majibu….. Huenda...

Dunia ina mengi tujitambue

Kalamu Ya Urithi Ya dunia   Huwenda hukuwa na utambuzi mzuri juu ya ile kauli isemayo kuwa uyaone. Huenda ni utoto tu na ujinga wa kipindi kile  ukiwa mdogo na ndiyo maana uliamini kuwa siku ukiwa mkubwa utakuwa na maisha mazuri. utakuwa ni mtu maarufu sana, na utapendwa karibu na kila mtu, utasaidia kila mwenye uhitaji. Na kubwa kuliko utakuwa na mpenzi mzuri mwenye kumjali na hata mkawa ni watu wenye kupendana sana. Lakini kumbe haiko hivyo…. Mambo hubadilika siku hadi siku. Na hata hivyo haikuwa rahisi kwa wewe kuamua ni aina gani ya maisha uyaishi ili hali wakati huo ulikuwa nimdogo sana na kwa bahati mbaya haukuwa na nafasi ya kufanya maamuzi kwa wakati huo. Zaidi ulikuwa ni tegemezi kwa kila kitu kipindi chote cha makuzi yako hadi kufikia sasa. Na sasa ni ni mtu mzima…. Unajuwa baya ni lipi na lipi ni zuri…. Kwa sababu hiyo, hatima ya maisha yako ya baadae huwa yapo mikononi mwa walezi wako. Hata maisha unayoishi leo ni juhudi za walezi wako. ...

Shairi : Chini Ya Jua

Kalamu Ya Urithi Chini ya Jua Chini ya jua Kunawatu wanaishi kwa kutegemea dhiki za watu… Kwao utu si kitu Kwao pesa ndo kila kitu.   Ni chini ya jua…. Mengi utayatambua Huko hakuna siri kila kitu ni dhahili.. Chini ya jua…. Huku ukitaka kumjua asiyekupenda Basi patwa na shida…   Chini ya jua Kuna viumbe hupenda kuishi kuliko kufa Uzushi kuliko taarifa Raha kuliko tabu…. Chungu kuliko tamu Huko chini ya jua Vya haramu ndivyo vinaumuhimu…. Chini ya jua Watu wanapenda uzinzi kuliko kazi… Watoto wa nje ni wengi kuliko wa ndani. Akiba ni ndogo kuliko madeni.   Chini ya jua rushwa ni bora kuliko kula Huku wengi huamini sana kulogwa kuliko kugongewa Wengi wao ni wazawa waliojiweka utawa Huona raha wakisifiwa Hawaoni ajabu wakidaiwa.   Chini ya jua… Kuna viumbe wa ajabu sana Hawa aibu hawana.. Wao kwa wao huchapana Mikia kulishana Nyonga kushikana Hawachelewi mapajani kuwekana. Chini ya jua. Lit...

Ushairi : Maumivu

Kalamu Ya Urithi Maumivu Chriss..! ''Yes kili…! Mambo vp brother… ''Fresh tu Mbona kinyonge sana ''Maisha tu kaka…'' Yeah ni kweli   but haupaswi kuwa katika hii hali. Brooo kuna vitu vinanichanganya ujue'' Vitu gani hivyo ''Broo ni kuhusu haya maisha.'' Chriss unajuwa sikuelewi…… nambie tatizo nini? ''Broo hivi   unaweza kuyavulia nguo maji na usiyaoge'' Hapana so rahisi kiivyo. ( Kimya kidogo )   Chriss   najuwa unachokifikiria But ni muhimu tukavumilia Naelewa magumu unayopitia Naelewa ndio….   ''Binafsi nahisi nimekuwa jaribio la kila tatizo Na kama ni kapu basi ni lile kapu la taka za uozo Sijakuelewa nini unachomaanisha? Broo sina furaha…. Sina raha… Na sijui ni lini nitaondokana na huu ufukara….''   Chrisss…. Natambua……. Natambua ni kwa vipi ufukara unakera… Ila fahamu huwezi kuwa na furaha kama huna hela Na hauwezi kuwa na hela ka...