Shairi: Uhuru gani huu

 

Uhuru gani huu?

kama maendeleo yatapimwa kwa mzani

unahisi afrika itakuwa na majibu gani

najiuliza

hivi ni nani alochimba shimo chini

kuzifukia hizi mila na tamaduni

eti akaziita ushetani.

Je ni sisi watu wa gizani au wale watu wa motoni

 Lakini kwanini tuliwaamini

Tukawakaribisha kizimbani.

 

Kwanini hatukuwapeleka utumwani…

Kwanini hatukuwapeleka vitani.

Kwanini tuliwaita wageni na si mashetani

Hivi walijikuta akina nani.

 

Kwanini hatukuwachapa viboko

Kwanini hatukuwashika madako

Kwanini hatukuthamini matambiko

Je haya ndo yale mabadiliko

Na je ni bora kuliko tutokako.

 

Kwanini iwe ngumu kwa wenye ardhi

Kwanini iwe vigumu kupata kazi

Au tupo dunia ya maradhi

Dunia isiyozingatia utamaduni wa mavazi.

 

Dunia isiyotafuta radhi

Wala heshima za wazazi

Dunia ya mababu wasokuwa na hadhi

Eti miungu ni upuuzi.

 

Dunia isiyo jali usawa wala uwazi.

Mweupe  mgeni ila mweusi mkimbizi

ardhi iliyolithi mila za kipuuzi

mila ya ushoga na usagaji.

 

Hivi ni nani huyo mlogaji

Alotuloga hadi akili

Leo tumewasahau wapolaji

Wezi na makatili

Leo tunaaita wawekezaji

Leo tunawaita watarii

Mbona mimi siwaelewi.

 

Hawa si ndo wale walobaka mabibi zetu

Kisha wakawabebesha vitu

Wakawatembeza kwenye misitu

Tena yenye miba bila viatu

Ni viumbe wenye roho za chatu

Ni binadamu wasio na utu.

 

Ewe mwana wa afrika

Kumekucha sasa amka

Ewe mwana wa nyika

Acheni sasa kutawanyika

Maana wakati umefika

Wa sisi sote kubadilika.

 

Enyi kizazi cha nyoka

Mlodanganywa mmelaanika

Huu ndo wakati wa sisi kuamka.

 

Hivi kwanini tusingewafanya misukule

Kisha tukawanyima shule

Badala ya tatuu tukawachanja chale

Watakaoleta ubishi tungewapiga mishale

au magobole ili  wakafie mbele.

 

hivi ni kweli waafrika tumesahau

au ndo kujisahaulisha

hivi ni mkweli walio tudharau

leo tunawaheshimisha

leo hii tunawaita wadau

wakati wao ndo walotufukaraisha.

 

mko wapi mashujaa wa aunika na unika

wazalendo wa kiafrika

mashujaa mlopewa madaraka

sasa mnakosaje mamlaka

wakati mnajuwa fika

ni wapi mlipotoka

maisha ya utumwa na patashika.

 

Enyi wasaliti wapenda noti

Mnakubalije kutumika

Enyi walamba nyayo washika goti

Ni lini mtaja badilika

Mkaachana na kuwa vizingiti

Mrudi nyumbani mnahitajika

Kwa pamoja tujidhatiti

Ili afrika iweze kubadilika.

Maana kutumika unika tumechoka.

Tafadhari rudini mlikotoka

Sasa kizimbani mnahitajika.

 

Wanauwa vipaji,  kwa kutunyima kazi

Wameruhusu ulaji,  kuua vizazi

Wamekuwa wanyonyaji , wamepandikiza mizizi

Hatuna msemaji,  afrika haina mkombozi.

 

Nauliza mko wapi wazalendo wa kweli

mko wapi mfano wa magufuli

Mko wapi enyi majasiri

Mashujaa msioogopa kabuli.

 

Hivi hadi lini tutakubali

Kuwa vibaraka wa nchi zao

Mbona imekithili hii hali

Kupangiwa bei za mazao

Tunaibiwa rasilimali

Zinaenda kwenye mataifa yao

Kwanini serikali

Hamfanyi kama wao.

 

Rushwa na ufisadi

Sasa mmegeuza ndo miradi

Pesa na majumba ya ablodi

Afrika kuipigisha hodi.


Na kilimboka

 

 

 

 

 

 

 

Maoni