Dunia ina mengi tujitambue
Ya dunia
Huwenda
hukuwa na utambuzi mzuri juu ya ile kauli isemayo kuwa uyaone.
Huenda ni
utoto tu na ujinga wa kipindi kile ukiwa
mdogo na ndiyo maana uliamini kuwa siku ukiwa mkubwa utakuwa na maisha mazuri.
utakuwa ni
mtu maarufu sana, na utapendwa karibu na kila mtu,
utasaidia
kila mwenye uhitaji.
Na kubwa
kuliko utakuwa na mpenzi mzuri mwenye kumjali na hata mkawa ni watu wenye
kupendana sana.
Lakini kumbe
haiko hivyo….
Mambo
hubadilika siku hadi siku.
Na hata
hivyo haikuwa rahisi kwa wewe kuamua ni aina gani ya maisha uyaishi ili hali
wakati huo ulikuwa nimdogo sana na kwa bahati mbaya haukuwa na nafasi ya
kufanya maamuzi kwa wakati huo.
Zaidi
ulikuwa ni tegemezi kwa kila kitu kipindi chote cha makuzi yako hadi kufikia
sasa.
Na sasa ni
ni mtu mzima….
Unajuwa baya
ni lipi na lipi ni zuri….
Kwa sababu
hiyo, hatima ya maisha yako ya baadae huwa yapo mikononi mwa walezi wako.
Hata maisha
unayoishi leo ni juhudi za walezi wako.
Iwe ni
kwenye mahusiano au hata katika shughuli za utafutaji bado walezi wako ndiyo
wenye kuashiria hatima ya maisha yako.
Maana wao
ndiyo wenye kukuandalia msingi wako wa maisha…
Hapa niwape
pole wale mlio na walezi ama wazazi wasiojitambua yaani vilaza…
Maana mzazi
mwenye kujielewa hawezi kushinda baa au kutwa akibadili wachumba, au mama kutwa
kubadili mitindo ya nywele na manukato ya bei ghali
ili hali
kizazi chake kinahangaika’’’
kinataabika…
mzazi
unashindania fashion za nguo, pikipiki,magari, namatoleo ya simu.
Na wakati
huo damu yake, mtoto wake, kijana
wake hana kazi hana mtaji wala hajui
afanye nini.
Kuna
wazazi, ni bora aweke bando la bukumbili
au tatu ili akeshe mtandaoni akichat lakini wakati huo mtoto wake hana vifaa
vya shule.
Huenda wewe
hapo unapitia magumu hayo kwa sababu
tu jana yako haikuwa nzuri…
Ndiyo…
jana yako haikuandaliwa vizuri na watangulizi wako.
Tazama…. leo
hii mahusiano yako yanashida kwa sababu huwenda umekulia katika malezi ya aina hiyo….
Baba mama
hugombana hadharani….
Ukiwa mtoto
huenda ulikuwa huku ukijuwa machafu ya tabia za wazazi wako.
Mtoto mdogo
kushirikishwa katika matukio kama usaliti, wizi, umbea , na hata uongo .
Lakini
haujachelewa….
Matendo na
tabia chafu zitaathiri maisha yako kwasababu ya uamuzi wako.
Uamuzi
utakaouchukuwa leo ili kuisahihisha kesho yako kutokana na makosa uliyokwisha
kufanyIka jana.
Chini ya jua
akitakacho mwelevu kiwe, basi kinawezekana
kuwa
Hatufanikiwi
kwasababu tunawekeza katika kushindwa
wamefanikiwa
kwa sababu hapo kabla walianguka mara kadhaa… na waliwekeza katika kufanikiwa.
hivyo mimi
nawewe tunapaswa kupitia mchakato huo.
Mchakato
ambao huenda ukaghalimu hata uhai wako…
Kuna kipindi
utagombana na kila mtu…
Kipindi
hicho utapoteza kila ulichokipenda…
Kila kitu
kwako kitabaki kuwa historia…
Na hapo
ndipo utaanza kuingia katika majaribu ya hapa duniani.
Kama ni
chungu ya maisha basi hapa ndipo utaijuwa….
Na hata ile
kauli ya dunia duara basi hapa ndipo mahala pake…
Aisee
tujifunze kuyaheshimu na kuyazingatia maneno ya watangulizi wetu yaani wahenga.
Ama kwa
hakika wakati huo hutakaa ukausahau kamwe
Wakati ambao
utabaki kama msindikizaji tu wa mafanikio ya wenzako….
Utakuwa na
wakati mgumu kiasi cha kujichukia…
Wakati ambao
utapaswa kukubaliana na kila hali
Wakati ambao
utapitia kila aina ya shida…
Tabu
Maumivu
Dharau,
Lakini
huwezi amini hicho ndo kipindi cha mimi na wewe kuweza kusimama tena
Hicho ndo
kipindi cha wewe na mimi kurekebisha tulipokosea..
Kipindi
ambacho kila kitu kitapaswa kuanza upya.
Uzima ni
zawadi ama ahadi isiyo na matumaini
ndani yake
Kwani
unaweza usiipate zawadi hiyo.
Na kama
ahadi hiyo itatimia basi kuna kila sababu ya kuwa watumiaji wazuri wa ahadi
hiyo.
Hivi
unatambua ya kuwa maisha haya bila wewe hayawezi kunoga…
Tena kama ni
chakula basi hakitakuwa na radha hata kidogo.
Raha ya
maisha uishi sambamba na wengine… uishi ukiona wengine wanaishi…. Wakuone
ukifurahia… uwaone wakifurahia pia.
Ukitembea
kama wao… ukilala kama wao… ukiamka kama wao… ukipumua kama wao…. Yaani wakuone
uwaone.
Na ikitokea
wewe uko na fura wao hawana hapo raha haitakuwepo…
Maana furaha
ya moyo hutegemea sana amani ya watu wakuzungukao.
Kwa maana
hiyo kasoro moja katika yote yaletayo uzima basi matokeo yake ni huzuni na hapo
maisha yako yatakuwa yameingiwa na dosari.
na Kilimboka
Maoni