Shairi : Mzalendo wa kweli

Kalamu Ya Urithi




Mzalendo

Naomba kuuliza swali

Hivi ni yupi mzalendo wa kweli

Kati ya raia mpigwa na askari kwa kudai maisha mazuri

Au polisi  hodari mwenye kuitii serikali.

 

Hivi nani mzalendo wa kweli

Kati ya raia alojiajili

Au mgombea msema kweli

Au masikini alotumia nauli kujengea kabuli  la tajiri

kisha akaikosa safari ya kwenda kuichukua miili ya marehemu wake muimbili.

 

hivi kweli taifa haliwezi kuwa na mashujaa wawili

kama ilivyo kwa kitendawili na methali kuwa kipimo cha wenye akili.

 

Eti

shujaa gani mponda mali

mzalendo gani baili

unajihitaje mtu wa watu wakati huna maadili

huna hekima wala ujasiri

huna shuhuda uliyemtoa mbali

akunadi mbele ya umma ili wakukubali.

 

Mnaoomba kula

mnauhakika gani kama tumekula

au ndo mnatuona mafala

tusiopenda hela au siasa biashara.

 

 aisee mnakosea sana

mnapoenda msirudi

na mnapokuja tena

eti mnafungasha vizawadi.

 

mnajisahaulisha mlichoahidi jana

kipindi hatuna maisha  hakuna anaye onekana

tukiwakumbusha  tunaanza kudanganyana

mnachosha afadhari yule wajana.

 

hivi kumbe ndivyo mnavyo fanya

baada ya kupata mlichotaka

haki zetu mnatuminya

mnasahau mliko toka.

 

mnafurahi mmezikusanya

kodi za raia walochoka

sasa hovyo mwazitawanya

jasho la mnyonge linatumika.

 

eti mnajiita mzalendo

wakati hamjui hata maana ya upendo

kutwa biashara za magendo

mnatabasamu sura kuficha matendo.

 

Haya sasa viti ni vyenu

Mnaojiita wazalendo wa jina

Haya sasa wakati ni wenu

Kula starehe za ujana

Mlizozikosa kile kipindi chenu.

Kipindi wazee wenu wakijichana

Wakati walipoifanya taifa lenu

Kuwa shamba la watwana.

 

Lini mtarudi nyumbani

Lini mtawakumbuka walio mashambani

Lini mtashika mpini kupima ugumu wa ardhini

Lini mtakaa barabarani  kuuonja utamu wa juani

Lini mtapita mashuleni au vyuoni Kuona wimbi la wakosa ajira mitaani.


Nauliza

lini mtaivaa miwani ili mpate kujiona mlivyo mashetani.

 

Unajiitaje mzalendo

 wakati ni mwoga wa kupambana

unajiitaje komando

wakati uoga wako tunauona

utashindaje kwa kishindo

wakati taifa lako halina vijana wenye elimu za maana.

 

eti yupi mwenye hasira

Yule anayechoshwa na ufukara

au Yule alochoka na kukaa jela.

 usinijibu…

ila naomba waambie wavutaji wa sigara

‘’acheni ufara…..’’

kuvutia kwenye mihadhara

kwenye mikusanyiko au daladala

waambie…

ila so kosa lenu

bali ni wale walio mbele yenu

maana hao ndiyo wanaokuza vichwa vyenu

kujiona wakishua kumbe waangukia pua

kujifanya mnajuwa

kumbe taratibu mnauliwa

 

mzalendo gani wewe

unayejipenda kuliko jilani yako

ufanye nini tuelewe,

wakati tunazijuwa tabia zako

kutwa kwenye vijiwe,

ukisengenya wenzako

msemaji mwenyewe,

usiye na hoja za mashiko.


na Kilimboka

 

 

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira