Shairi: Huoooooooo..!

Huooooooo!

Kaka hivi ulisema utaoa lini?

Kwa kosa gani?

Kwani kuoa ni kosa?

''Hujui kama ndoa ni kifungo''

So kweli wewe ni muongo

Kama utaniita mimi muongo je wenye ndoa utawaitaje

''Labda wazugaji''

Hapo Utakuwa na utani na wadangaji

''Kwaiyo ndoa ni pango la kufichia maovu yao''

kaka unautani na wenye ndoa zao

''Sio ndoa zao sema wenye vifungo vyao''.

Ha ha ha

 

''Kaka''

Masikio yapo wazi ongea

''Sawa, nasikia siku hizi jamaa anatembea na remote controller''

Usiniambie, ili iweje

''Umesahau''

Kaka unajipenda  kweli….

''Huooooooo''

aaa nimekuelwa.

 

Kaka

''Mbwa wewe nambie…''

Hivi nikiwa chawa wao si nitanenepa

''Eee utanenepa kama unakulaga nyumbani kwao…''

Kaka wivu huo…

''Wivu kitu gani mbwa wewe''

 

''Nawachukia sana''

 wananifurahisha mno

''Waliniunguzia tv yangu ya chogo''

Walinilaza gizani kama popo

''Ila wazuli kwenye makato na malipo''

Aaa.. mimi siwakubali hata kidogo…

 

''Kwanza.. hivi ada yao ni shingapi''

Hata sijui mainswitch yao iko wapi…

 

''Nasikia meneja wao anatumia nishati wa jua''

Kwani  solar na wao kipi bora

''bora jua….''

Maana giza likifika mwezi unawaka.

''Afu Wao wanazimika''

Ha ha ha ha

''Pumbavu zao''

 

Eti kaka hivi  mwanza ikikosa nyegezi itakuaje

''Labda tuwaulize ubungo bila stend wanaishije''

Nahisi jibu letu litakuwa mbezi…

''aisee sina uhakika….''

 

Kaka

 ''hivi kuna kitakachabadirika''

Lini au huu mwaka

''Kaka sikuhizi kila kitu kimebadilika''

Mbona mimi sioni

''Inamaana siku hizi hauoni basi vaa miwani''

Kaka huo utani

''Hivi kweli hupaoni''

Sioni wapi

''Kaka barabarani''

Kwani kuna nini

''Inamaana huoni… jinsi Ukimya ulivyotawala''

Acha uendelee kututawala  maana tulishakuwa mafala ….Mbwa siye

 ''Afu kaka''

Nakusikia….

 ''Siku hizi sisikii kelele za magari wala miungurumo kwanini''

Nikuulize wewe fundi unayejisifu kwa udereva makini

''Au barabara pana siku hizi…''

Nikuulize wewe mpita njia

''Kaka au umechukia kisa nilivyokuambia''

unatoa majibu au unaulizia…

 

''Mhhh kwahiyo hata honi hazipigi….''

Yaani ni mwendo wa mnyefu… Yaani ni mwendo wa kimya kimya

''Hahaha sikuhizi mji umekuwa na magari bubu…''

Kaka tatizo so magari bubu tatizo ni njia

''Zimepanuka.''

Kwani greda zimepita lini?

''Mbwa wewe… kawaulize wapita kwa miguu.''

 

Na vipi ukipita chocho

''Kaka huko ndo usiseme kusha kuwa dimbwi… wakabaji wengi Kuna foleni hadi za bajaji.. Yaani chocho hazitamaniki Panya road wamejaa kila kona…. Nahisi hata huko ni yale yale tu…''

Kwani askari hawapo….

''Kaka polis au patroo… naona hawausiki na huko''


kaka

''afu nimepata kazi''

kazi gani hiyo

''ni kazi ya kuchimba mitaro ya maji taka''

unakoelekea utaanza kufukua mitalo ya mavi taka

''bora tunaofukuwa  kuliko wanaofumua bomba za maji taka''

Sijakuelewa hapo…

''Kaka mimi huko simo''…

Huoooooooooo

''Duuu hawa nao kwa kujisikia''

Yaani saa hii ndo wanaturudishia

''wanakoelekea nitahama mtaa''

Uhamie wapi

''Dodoma''

Kwakumuogopa obama

''Au Yule binti osama''

Kaka huko jua halizami hovyo

''Kwakuwa huko ni mwezini au , mbwa wewe…….''

 

 

Kaka nina swali

''Ila usiulize kitendawili''

Hivi kunamaana gani nikisema hakombi mboga bila kulamba bakuli.

''Kabla sijakujibu''

Kwanza kamuulize mpishi eti kati ya kidole na bakuli kipi hulambwa kwa ulimi.

 

''Ujuwe sio pilipili…''

Utawashwa wewe….. hadi ukome

''Ujuwe sio mimi…''

 

''Hatari hiyo mboga haichagui ugali''

Umekubali eeeee

''Hapana labda wali hauchagui kachumbali''

So kweli

''Ni mboga ndo haichagui pilipili''

Ila mimi nahisi nyama choma

''Ndo inaendana na wali''

Hapana

''Inaendana na ugali''

Basi labda kachumbali….

''Wewe unasema nini…''

aaaaa hamna…

''Mbwa wewe''

 

Ila kuna wakati huo wako vizuri

''Aaa mimi siwakubali''

Kwa kukata

''Wamefanyaje...?''

Aaaa umekataaaaaaaa.

''Hawa nao hawana kazi za kufanya….''

Badala ya kukata mauno

''Wanakata waya''

Kaka hivi waya ukikatikia ndani  umeme utawaka kweli.

''Nahisi transfoma itafeli.''

 

Kaka hivi kwenu wapishi wanaruhusiwa kulamba mwiko

''Kwani nyie mnaruhusiwa kula kwa mwiko.''

Ni kosa kwa mila zetu

''Sisi ni dhambi kwa destuli yetu''

 

Kaka mimi nimechoka

''Umechoka nini..''

Nimechoka kufukuza mende

''Sasa wewe unaishije na mende''

Ndo nyumba za kupanga zilivyo tafanyaje

''Hauna dawa uwapulizie''

Kaka nimechoka kuwauwa

''Kaka huchoshwi na vifo vya mende''

Nichoswe vipi wakati sitaki hata niwaone

''Kaka mimi ujue nina huruma sana''

Hata nikimkuta mende nyumbani ameanguka chali

''Aisee lazima nimgeuze''

Sipendi atembelee mgongo muda mrefu coz nahisi kama anaumia vile..

''Acha ushamba wewe..''

Ungemuacha vilevile tena ungemkanyaga hadi afe….

''Kaka kuwa na huruma wewe…''

Nao ni viumbe…

''Sio kwa mende hawa sasa.''

 

Aisee kwani ni mende gani hao

''Si wale wakianguka chali hawawezi kujigeuza''

Kwani ni wale wakubwa au wadogo

''Kaka maswali gani hayo wewe juwa ni mende''

Basi chunga sana wasije wakawa wale mende wa maradhi.

''Ukaanza kuzunguka huku na kule ukitafuta tiba''

Kama ni hivyo mwakani najenga nyumba nzuri na ya kisasa

''Hayo ndo mambo.''


Kaka jenga nyumba yako hao mende sio…

''kaka unataka kusema kuwa wenye nyumba hawaishi na mende''

Kaka tueshimiane nimeoa juzi ujue

''Kaka nina habari mpya''

Ni mpya kweli .


''Nasikia sikuhizi vibogoyo wanang’ata nyama…''

Hiyo kuukuu leta nyingine

''Nasikia siku hizi wanaume wananyonya vidole''

Unashangaa nini ?

''Kwani wanawake hawanyonyi vidole''

Kaka vidole si wananyonya watoto….

''Sio watoto bali watoto wadogo.''

Una mpya nyingine


''Kaka nasikia siku hizi takataka hawamwagii ndani wanamwagia jalalani''

Unasema nini wewe?

''Sasa ulitaka wamwagie wapi''

Mbwa wewe…

''Wamwagie chooni''

Labda chooni kwako

''kaka usichukie nauliza tu…''

mbwa wewe.


Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Ushairi : Maumivu

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira