Ushairi : Maumivu

Kalamu Ya Urithi



Maumivu

Chriss..!

''Yes kili…!

Mambo vp brother…

''Fresh tu

Mbona kinyonge sana

''Maisha tu kaka…''

Yeah ni kweli

 but haupaswi kuwa katika hii hali.


Brooo kuna vitu vinanichanganya ujue''

Vitu gani hivyo

''Broo ni kuhusu haya maisha.''


Chriss unajuwa sikuelewi…… nambie tatizo nini?

''Broo hivi  unaweza kuyavulia nguo maji na usiyaoge''

Hapana so rahisi kiivyo.


(Kimya kidogo)

 

Chriss  najuwa unachokifikiria

But ni muhimu tukavumilia

Naelewa magumu unayopitia

Naelewa ndio….

 

''Binafsi nahisi nimekuwa jaribio la kila tatizo

Na kama ni kapu basi ni lile kapu la taka za uozo

Sijakuelewa nini unachomaanisha?

Broo sina furaha…. Sina raha…

Na sijui ni lini nitaondokana na huu ufukara….''

 

Chrisss…. Natambua…….

Natambua ni kwa vipi ufukara unakera…

Ila fahamu huwezi kuwa na furaha kama huna hela

Na hauwezi kuwa na hela kama hauna nyenzo bora

Chrisss naomba uutulize moyo

Naomba usifikilie hayo

Kwa maana mungu si mchoyo

Kama binadamu tulivyo.

 

''Hapana kili

Ujuwe hili linaniumiza sana akili.

Maana kila nikifikili

Naishia kuzalisha maswali

Kuwa hivi ni kweli

Kwa hii elimu yangu nilistahili

Kubebelea tofari.''

 

Nooo chriss usiseme hivyo…

Just ni suala la muda tu…

Ni kweli kazi ndo kila kitu

Najua kazi nzuri hujenga heshima ya mtu

Na tena  ni kipimo cha utu

lakini jambo hili haliitaji haraka….

 

''Hapana kaka…

Kuna wakati nachoka

Natamani nirudi kule nilipotoka

Mwa mama tumboni

Au kule utotoni

Huenda sitojuwa ya duniani.''

 

Sio rahisi kiivyo

Na hata hivyo hayo ni mawazo ya kitoto

Hivi ulisha tembelea mahospitalini ukawaona walio na matatizo

Watu walio elemewa na changamoto

Tena zaidi yako

Mhhh  hivi ulishafika mahakamani na polisi ukaona watu wanavyokula msoto

Au omba omba mtaani

Yatima wasio na matumaini…

Ambao hawajui ni lini wataipata hauweni.

 

Please chriss just calm down…

Naomba uamini kuWa zamu yako ipo mbioni

Na kama si kesho basi tarajia siku za usoni.

 

''Kili unasema nini

Ni mara ngapi tunalala njaa bila chochote kitu tumboni

Mhhh ina maana hauoni

Mhhhh ni mwaka wa ngapi toka utoke chuoni

haya una kazi  gani….

Mhhh huoni….

Tutaishi hivi hadi lini?

Eti kili..!

nijibu hili swali

tazama wengi huko wanatanua

huku mimi na wewe tunapigwa jua

haulioni hili…''

 

chriss

kwahiyo unatakaje…

tukavunje…

sema…

tukaibeeee

ili tukamatwe

tupigwe mawe tufe

au polisi watushike

kisha tufungwe

ni vipi kuhusu ndoto zetu

au ndo umesahau kila kitu

 

sasa nani alaumiwe..

je wazazi au serikali

au wewe…

sema….au jamii nzima

kwa kosa la kukubali

 mitaala isiyo na ukweli

au tulaumu wabunge matapeli

viongozi wasio na maadili….

Eti sema

 

Chriss me nafikiri

Tuendelee tu na hii kazi ya tofari

Huwenda siku moja itatupa utajiri

 

''Sawa kili

Nimekuelewa''

Basi vizuri kama umenielewa

Acha tuendelee na kazi

 

na Kilimboka

Maoni

Mashairi Pendwa Zaidi

Shairi: Kipenzi changu

Shairi: Moyo Wa Subira